The House of Favourite Newspapers

Lamar amtimua Khloe Kardashian Hospitali

0

Staa wa kikapu Lamar Odom.

WAKATI ikielezwa kuwa Khloe Kardashian amekuwa karibu na staa wa kikapu Lamar Odom ambaye amelazwa, habari ni kuwa Odom amemtimua mrembo huyo ambaye ni mke wake kutoka hospitali kutokana na kutumia ugonjwa wake kujipatia umaarufu.

 Khloe Kardashian.

Taarifa zinaeleza kuwa mara baada ya Lamar kupata nafuu na kujitambua, alipata malalamiko ya kuwa Khloe anatumia hali ya ugonjwa wake kujiongezea umaarufu na ndiyo maana yupo karibu naye muda mwingi licha ya kuwa walikuwa mbioni kutalikiana rasmi.

Odom amelazwa hospitali tangu wiki iliyopita baada ya kuzimia ghafla akidaiwa kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya.

Leave A Reply