The House of Favourite Newspapers

Lamar Odom hatihati kupona kwa kutumia madawa ya kulevya

0

Lamar (2)Mchezaji maarufu wa  mpira wa kikapu wa Marekani, Lamar Odom akiingizwa kwenye gari kupelekwa hospitali kwa matibabu.
Lamar (3)Lamar Odom akiwa na baba yake, JoeLamar (4)Lamar Odom akiwa uwanjani
Lamar (5)Lamar Odom na aliyekuwa mkewe, Khloe Kardashian.
Lamar (6)Lamar Odom na familia yake.Lamar (8)Aliyekuwa mke wa Odom, Liza.
Lamar (9)Liza na baadhi ya wanafamilia wakienda kumuona Lamar OdomKimKim Kardashian akiwasili hospitali ya Sunrise iliyopo Las Vegas, Nevada alikolazwa Lamar Odom.
Lamar (11)Shangazi yake Lamar aliyemsomesha shule ya Queens huko New York, NeanMerecer naye akienda kumjulia hali mwanaye huyo.
Lamar (12)Joe akielekea kumuona mwanaye Lamar.
Lamar (13)
Lamar (14)
Lamar (1)Chumba alichopanga Lamar kabla ya kupatwa na matatizo hayo.

MCHEZAJI maarufu wa  mpira wa kikapu wa Marekani, Lamar Odom, amelazwa hospitali huko Las Vegas tangu Jumanne wiki hii akiwa mahututi baada ya kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi, limetaarifu gazeti la  Daily Mail Online.

Odom, mwenye umri wa miaka 35, hivi sasa anapigania maisha yake kutokana na kutumia madawa hayo kwa muda wa siku nne akiwa katika hoteli moja na makahaba huko Nevada.

Khloe, mke wa Odom, ambaye ni dada mkubwa wa mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, akiwa kando ya kitanda cha mumewe huyo, alisema kurudia tena kwa Odom katika utumiaji wa madawa ya kulevya huenda kunatokana na kifo cha rafiki yake mkubwa, na huenda alikuwa anataka kujiua.

Hospitalini hapo, Khloe aliungana na dada yake Kim ambaye kwa sasa ni mjamzito, na mama yake,  Kris Jenner.   Wengine waliofika hapo ni mpenzi wake wa zamani, Liza Morales, na watoto wao wawili Destiny (17), na  Lamar Jr (13) waliofika hapo kutoka New York.

Khloe ndiye anayeamua mambo yote ya tiba ya Lamar hospitalini hapo, japokuwa wawili hao wamesaini hati za kutalikiana ambazo bado hazijakamilika mchakato wake, ikimaanisha kwamba bado wangali mke na mume.

Tangu afike hapo Jumanne usiku, Khole hajaondoka hospitalini hapo.

Madaktari wamesema waligundua kila aina ya madawa ndani ya mwili wa Odom ambapo vyanzo vingine vilisema alikuwa amekumbwa wakiongeza kwamba matumaini ya kuishi kwake yalikuwa nusu kwa nusu na kwamba akipona huenda akapatwa na matatizo ya ubongo.

Leave A Reply