Kartra

Lamine Moro Awaita Mashabiki kwa Mkapa -Video

NAHODHA wa Yanga, Lamine Moro sio mchezaji wa kukata tamaa katika majukumu yake, ameyasema hayo kuelekea mchezo wao dhidi ya KMC utakaopigwa kesho Jumamosi ya Apri 10, 2021 kwamba wapo tayari kwa mapambano.

Moro ameyasema hayo leo Ijumaa, kwamba wamejiandaa vya kutosha wana imani kwamba watanyakua pointi tatu katika mchezo huo.

 

“Tangu nijiunge na Yanga sijawahi kuona mechi rahisi, kila tunapocheza ushindani unakuwa wa juu, lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu hilo ndilo jambo la msingi kwetu,” amesema na ameongeza kuwa;

 

“Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kutuunga mkono, naamini hatutawaangusha tutapambana kwa kadiri tutakavyoweza kwa ajili ya kuhakikisha timu yetu inaendelea kuwa kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu,” amesema.


Toa comment