Kartra

Lamine Moro, Yanga Waitwa Mezani

MWENYEKITI wa Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza), Mussa Kissoky amesema kuwa wanawakaribisha Yanga na Lamine Moro mezani kujadili matatizo yao.Hii ni baada ya Lamine kutoa malalamiko ya kudaiwa na klabu yake kuwa ana utovu wa nidhamu.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kissoky amesema kuwa: “Mpaka sasa hatujapata malalamiko yoyote kutoka Yanga wala kwa Lamine Moro, ila kama wameshindwa kuzimaliza tofauti zao waje mezani tutawasikiliza.

 

“Nachukizwa sana na baadhi ya klabu wanavyoficha maovu ya wachezaji wanapoonyesha utovu wa nidhamu, hakuna mwana michezo duniani aliyefanikiwa bila kuwa na heshima, waache hiyo tabia ya kuangalia ukubwa au umaarufu wa mchezaji. “

 

Halafu kuna suala limezuka kwa baadhi ya klabu mchezaji anapodai stahiki zake anaonekana hana nidhamu, naomba viongozi waangalie hili maana ni haki ya mchezaji kupata haki yake.”

STORI: CAREEN OSCAR, Dar es Salaam


Toa comment