Lamine Rasmi Nahodha Mpya Yanga

YANGA Oktoba 8, 2020 uongozi umetangaza rasmi beki Lamine Moro kuwa nahodha wao mpya akichukua nafasi iliyoachwa wazi na kiungo Papy Tshishimbi.

 

Tshishimbi ndio alikuwa nahodha mkuu wa mwisho katika kikosi hicho mpaka msimu uliopita unamalizika lakini baadaye aliachana na klabu hiyo baada ya kushindwa kukubaliana na viongozi wa klabu hiyo katika kuongeza mkataba mpya.

Moro ambaye juzi tu aliongeza mkataba wa kuendelea kusalia katika klabu hiyo kuwa nahodha wao mpya akiwa ameanza vyema msimu huu.

 

Mbali na Moro pia beki mwenzake pacha Bakari Mwamnyeto naye amepewa unahodha msaidizi katika majukumu hayo.

Mabeki hao ndio wanaongoza safu ya ulinzi ya Yanga ambayo mpaka sasa katika mechi tano ndio ukuta pekee umeruhusu bao moja pekee huku pia Moro akifunga mara mbili katika mechi mbili tofauti.


Pia taarifa hiyo imemtaja kiungo Mukoko Tonombe kuwa nahodha wa tatu akimsadia Moro ambapo mkongomani huyo akiwa ameanza vyema msimu huu wake wa kwanza ndani ya Yanga akiwa na bao moja huku pia akitoa pasi moja ya bao.

 

Hatua hiyo ya Yanga ni kama inawaongezea morali zaidi wachezaji hao watatu wanaocheza eneo la ulinzi katika kuiongoza timu hiyo kuwa bora zaidi katika ukuta wao msimu huu ambao hawajapoteza mechi yoyote zaidi ya kutoa sare moja na kushinda mechi nne.

Toa comment