LATRA Yasitisha Leseni ya Kampuni ya Mabasi ya KATARAMA
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani imefanya kikao na wasafirishaji wa mabasi ya Mkoani ili kuwakumbusha kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani.
Aidha, LATRA imesitisha Leseni ya kusafirisha abiria kwa kampuni ya mabasi ya KATARAMA Luxury kutokana na kuchezea kifaa cha kufuatilia mwenendo wa magari (VTD)
Kufuatia kikao hicho, Mamlaka imetoa onyo kali ya wiki moja kwa ABOOD Bus Service, BM Coach na SUPER FEO kwa kosa la kuchezea mfumo wa mwenendo wa magari (VTS) na kukiuka masharti ya leseni walizopewa na kuwataka wasafirishaji wote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.
Kikao hicho kimefanyika Ofisi ya LATRA Dar es Salaam, Septemba 12, 2024 na kuhudhuriwa wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania (TABOA), Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, pamoja na Wamiliki na Wawakilishi wa Makampuni hayo.