LATRA Yatangaza nauli za abiria wa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar Mpaka Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora ambapo abiria anayetoka Dar es Salaam hadi Dodoma atapaswa kulipa Sh 31,000.
Kiasi hiki ni chini ya gharama ambazo mabasi mengi yanatoza kwa safari kama hiyo. Bei ya chini kwa basi kama la Shabiby ni Sh 29,000.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano LATRA, Salum Pazzy amesema tangazo hilo linafuatia maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusu maombi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali.