The House of Favourite Newspapers

Leila: Kitawaka Dar Live

0

NA MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA | OVER THE WEEKEND

MALKIA wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid amefunguka kuwa tofauti na mara zote ambazo bendi yake imekuwa ikifanya maonyesho huko nyuma,

katika onyesho ambalo italifanya Jumamosi ya mwisho ya mwezi huu, April 29, katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem imepania kuwasha moto na kuacha  historia.

Akichonga na Over Ze Wikendi, Leila alisema katika onyesho hilo ataibuka na manjonjo tofauti stejini ambayo  yatanogesha  burudani usiku huo  na amewataka  wapenzi wa Muziki  wa Taarab na wapenda  burudani kuibuka siku  hiyo bila kukosa.

“Hiyo siku  kitawaka Dar  Live, siwezi kuweka  wazi kila kitu  nitakachofanya  lakini kiukweli itakuwa  tofauti sana na  ilivyozoeleka kuwa  huko nyuma. Onyesho  hili nimejipanga mno  kuhakikisha wapenzi wa  bendi yetu na wapenda  burudani wote wanapata  kitu roho inapenda,”  alisema Leila.

Malkia huyo aliongeza kuwa mbali na yeye kuwasha moto, lakini pia atakuwa sambamba na wakali wengine wa Jahazi wakiwo Amigo, Mwasiti Kitolonto, Ally J, Fatuma Kassim na wengine wengi.

Naye Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa kiingilio katika onyesho hilo ambalo litaacha historia Dar Live kitakuwa ni shilingi 6,000 tu.

“Naimani kabisa mashabiki wa burudani wanafahamu nini Jahazi huwa inawapa, kwa hiyo niwatake kufika bila kukosa.

Hata hivyo, mbali na onyesho hilo la Jahazi, mwezi ujao tarehe 6, kutakuwa na onyesho babu kubwa la Christian Bella atakayesindikizwa na Pam D pamoja na Gigy Money,” alisema Mbizo.

Meneja huyo alimalizia kuwa ukiachana na Bella ambaye mara ya mwisho amepiga shoo Dar Live mwaka 2015, mwezi huohuo kutakuwa na tamasha la Nay wa Mitego linalokwenda kwa jina la Wapo. Ambapo Barnaba, Shilole, Dullah Makabila watamsindikiza huku Shamsa Ford akiwa ni ‘special apearence.

SHOO YA HARMORAPA, JUMA NATURE, MSAGA SUMU, DULA MAKABILA DAR LIVE

Leave A Reply