testiingg
The House of Favourite Newspapers

Leo Kazi Anayo, Mastaa Wamvaa Aristote

0

MASTAA mbalimbali wa filamu na muziki Bongo, wamemjia juu Aristotee kufuatia kauli yake aliyoitoa kwa Wema Sepetu kwamba “miaka yote hana hata gari bado ana-request uber… huku akidai kuwa mrembo huo anazidiwa pesa na uzuri na Irene Uwoya…”

 

Mastaa ambao wamemrarua Aristotee ni pamoja na DC wa Temeke, Jokate Mwegelo, Shilole, Hamisa Mobetto, Rubya, Shetta, Juma Lokole na wengine wengine.

 

Katika taarifa zao zilizoonesha wakiungana na #Wema wengi wametafsiri kauli au kitendo cha #Aristote ni kejeli na dharau kwa mwanamke.

 

Wema Sepetu

Wacha nikuweke kabisa kwa page yangu upate kufurahi… maana nimekaa sana mdomoni mwako…. Kutwa huishi kunitaja….

 

Kurequest nako ni K vile vile maana nakutanaga na mashabiki pia nikiwa kwenye Uber na Bolt… And by the way, miaka miwili sasa sina gari na mbona maisha fresh tu… Mkitembelea nyinyi ma Range inatosha Aristotee… Sio mbaya….🙏🏼🙏🏼🙏🏼

Ila ifike muda mnipumzishe basi maana Im nat in a competition na mtu yoyote in my life… Niko na deal na Wema wangu tu… Sijawahi kushindana na mtu… Always stood on my own…. Nashkuru…
FAIZA ALLY

Wote tumepost wema sawa basi tuchukue action mimi naona tukiamua kumchangia wema laki moja kwa sisi maarufu na wa Tanzania wengine wenye mapenzi binafsi wako wengi kwa uwezo wao mbona Wema anapata gari tu fasta tena.

 

@directorjoan @jokatemwegelo @diamondplatnumz @auntyezekiel na ma Star wengine kibao hili linawezekana hlf niwambie kitu insta asingekuwepo wema kusinge damshi kivile mie binafsi na mapenzi mengi tu basi kama vipi tuchukue action.

 

Mlio karibu nae nyie watu wa karibu wa wema @petitman_wakuache @martinkadindaofficial ongeeni nae akikubali hilo mbona week kabla haijaisha wema ana bonge la gari Kama shida ni gari …. Wema ana nguvu ya watu wengi sana sasa ndio wkt wa kuonyesha nguvu yenu kwake sio tuishie kwenye kupost now tu take action #wemakipenzichawatanzania.

 

Shilole

“Jina WEMA ABRAHAM SEPETU litamkwe kwa heshima. Heshima kubwa kama wanayostahili mabinti wote wa Kitanzania (Hakuna mtu anatakiwa kukejeliwa au kushambuliwa mtandaoni), heshima kubwa ya utu wa kweli, na Heshima kwa huyu ni WEMA. Tanzania’s Sweetheart atabaki kuwa Sweetheart wetu milele. @wemasepetu We love you❤️❤️❤️. #RespectKwaWema #WemaMoyoni

 

Shetta

“Moja ya ukatili mmbaya duniani Ambao Umeleta matukio mengi ya kutisha na unaendelea kusaabisha mambo mengi ya Hatari katika maisha yetu sisi hapa duniani ni Ukatili wa kihisia na Ukatili wa Kimtandao, upelekea mpaka vifo muda mwingine. Watu wanajiua kwa ukatili wa namna hii.

 

Tushasikia sana watu wengi wamejiua, wengine kupoteza direction ya maisha kabisa kutokana na haya mambo.

Naomba nitoe rai tu kama kijana ninaependa kuona tunakua na Usawa wa kijinsia kwenye jamii na kupinga Ukatili hasa kwa wanawake na watoto. Ifike mahala sisi kama vioo kwenye jamii tutumie umaarufu wetu kwenye kuelimisha mambo haya yasitokee, na tusiwe mstari wa mbele kufanya sie ndo chachu ya kufanyiana ukatili.

 

Nimeliona hili la dada yangu @wemasepetu linaloendelea kwenya mtandao, na niseme tu Kwa niaba ya shirika letu la @sawa_tanzania Tunakemea vikali zaidi Ukatili hasa ukatili wa Mitandaoni (online Bullied).

 

Ni jambo kubwa kaka yangu @aristotee amefanya kuomba radhi, Ila Iwe funzo kwa watu wengine wote, Tunaweza kuona ni jambo la kawaida kumbe tunasababisha mambo makubwa kwenye maisha ya mtu mwingine. (Victim) #StopOnlinebullying. Cc @sawa_tanzania @wemasepetu 🔑

 

Jokate Mwegelo; Ifike muda sheria ifuate mkondo wake kukomesha tabia na hulka za aina hii kwenye jamii zetu. Iwe funzo kwa wote. Na msamaha pekee yake hautoshi. Watu wanajiua kwa kuwa bullied online. This has to stop!!! I believe you will do the necessary @wemasepetu @bestizzo @martinkadindaofficial 

 

Wolper

Mfalme sulemani alikuwa sahihi sana kuomba HEKIMA kuliko utajiri,ama mengineyo ambayo yanaonekana kama ndio furaha ya maisha hapa duniani… Kabla ya kuomba yote na Hekima ni kiwe kitu cha kwanza pia maana ukiwa na hekima unakuwa na vyotee.

 

Tupendane ktk ukweli bila unafki na pia haya maisha ya mitandao yasitufanye tuone ndo mwisho wa kila kitu maana tunahitaji kujifunza vingi vizuri kuhusu maisha kabla ya kutafuta tunavyovitafuta huku mitandaoni.

 

Pesa sio kila kitu na hata wanaokosa pesa hawajakosa vitu vingine… Kiburi cha uzima kisitufanye tusahau hapa duniani tuwapitaji,tusiumizane kwasababu ya kipato au maneno ya kuharibiana siku.
#OgopaKuwaSababuYaMwenzioKulia

Leave A Reply