R.O.M.A Mkatoliki
BAADA ya kusubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Muziki wa Bongo Fleva, Singeli, Taarab na Mduara hatimaye imefika ambapo leo wakali R.O.M.A Mkatoliki na Snura watakuwepo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kukamua mwanzo mwisho.
Akizungumza na Risasi Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa shoo hiyo itatambulika kama Usiku wa Nani Mkali ambapo burudani itafunguliwa rasmi saa mbili ya usiku.
Snura
“Mashabiki watarajie burudani kambambe kutoka kwa wakali wa Singeli wakiongozwa na Man Fongo na Shoro Mwamba ambao watapiga ngoma zao zote za Uswazi kuanzia Hauna, Hainaga Ushemeji na Sembe Tembele,” alisema Mbizo.
Mbizo aliongeza kuwa;
“Snura ambaye ni mkali wa Mduara atakuwepo kutambulisha staili mpya ambayo itakuwa sapraiz kwa mashabiki wake huku naye mkali wa Hip Hop, R.O.M.A akiwapagawisha na ngoma zake kali kuanzia kuanzia Mathematics, 2030, Mtoto wa Kigogo na nyingine nyingi.
“Burudani haitaishia hapo, tutakuwa nao wakali wa Muziki wa Taarab, Mashauzi Classic wakiongozwa na Isha Mashauzi ambao watapagawisha na vibao vyao vingi ambavyo ni Mapenzi Hayana Dhamana, Mapenzi Yamenivuruga na Nimpe Nani.
Burudani hiyo itakayokwenda kwa kiingilio cha 8,000 tu getini, imedhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money Tap Tap.