The House of Favourite Newspapers

Leo Tigo Ilivyogawa Mamilioni na Vifaa vya Hisense Kwa Washindi wa Ndinga la Kishua

0

Dar es Salaam, 6 Januari 2023:Mwenye bahati habahatishi: Ndivyo ambavyo unaweza kusema wakati Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ilipokuwa ikiwapa zawadi zao washindi wa droo ya sita ya Kampeni ya Ndinga la Kishua walioibuka washindi katika kufanya miamala ya Tigo Pesa.

Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kushoto) akimpongeza mshindi wa Vifaa vya Hisense, Madielo Mai (kulia) kulia ni Afisa Masoko wa Hisense, Joseph Mavula.

 

Akizungumza kwenye hafla ya utoaji zawadi hizo jijini leo, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema;

“Leo tunayo furaha kutoa zawadi kwa washindi wa droo ya sita na mpaka sasa zimebakia shilingi milioni 46 kugawa kwa washindi wetu kwa wiki mbili zilizobaki ambazo ni milioni moja moja kwa wiki ambapo tutazigawa kwa wiki mbili pamoja na milioni kumi ya mshindi mkubwa na milioni ya mshindi mkubwa pia.

Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kushoto) akimpa mfano wa hundi, Joanitha Mnigo baada ya kujishindia kitita cha shilingi milioni moja.

 

“Mbali na hayo kuna zawadi ya Ndinga la Kishua aina ya Toyota Rush jipya kabisa ‘ziro kilomita’ ambayo inamsubiria mshindi wa mwisho wa kampeni hii na pia kuna vifaa vya Hisense kila wiki tunaendelea kuvitoa.

“Kama nilivyosema zoezi hili limebakiza wiki mbili hivyo watumiaji wote wa simu za mkononi nawasihi kutumia mtandao wa Tigo ili muweze kupata huduma za Tigo Pesa kufanya miamala mbalimbali ili uweze kuwa mshindi wa zawadi hizi zinazoendelea kutolewa.

Mshindi wa vifaa vya Hisense akikagua vifaa alivyojishindia kabla ya kubeba vifaa vyake.

 

“Ili kujishindia zawadi hizi fanya miamala mingi uwezavyo kama vile kulipa bili, kutuma na kupokea pesa, kupokea na kutuma pesa kutoka benki au mitandao mingine au nchi za nje pamoja na kufanya malipo ya serikali chukua mikopo kutoka huduma yetu ya Nivushe na Bustisha ili ujiongezee nafasi ya kuwa mshindi”. Alimaliza kusema Mary.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya Hisense, Joseph Mavula amesema;

“Siku ya leo ni muendelezo wa ugawaji wa zawadi wa Kampeni yetu ya Ndinga la Kishua, Mamilioni ya pesa na Vifaa vya Hisense ambapo wiki hii tuna jumla ya washindi wawili waliojishindia vifaa vya Hisense ambavyo ni TV nchi 50, friji, microwave pamoja na spika za muziki za kisasa yaani sound bar.

“Lakini pia tuna nafasi nne za washindi kwa wiki ijayo na inayofuata pia hivyo nafasi ni yako fanya miamala ya Tigo Pesa kwa wingi kadri uwezavyo ili uweze kuibuka mshindi.

“Vilevile nawakumbusha wananchi wote kutembelea maduka yetu yote ya Hisense hapa nchini kujipatia bidhaa zetu kwa ofa yetu ya punguzo la asilimia 20 ambayo bado inaendelea.

Leave A Reply