LEO TUNAFUNGA JUMLA JUMLA 2018 ROSTAM, MAUA SAMA DAR LIVE

 

WAKALI wawili wasioshikika kwenye Muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki pamoja na Stamina wanaounda Kundi la Rostam pamoja na mwanadada, Maua Sama wamesema kuwa, kuelekea mkesha wa Mwaka Mpya watahakikisha wanafanya shoo ya kufuru inayotambulika kama Tunafunga Jumla Jumla, Desemba 31, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.Akizungumza na Risasi Jumamosi, Roma alisema, kila mwaka huwa habahatishi katika kufanya shoo za kufunga mwaka.

“Kama mtakumbuka katika mkesha wa Mwaka Mpya ile mwaka jana niliingia na ‘crane’ ambayo ilinibeba juu na kunishusha ndani ya Dar Live katika shoo ya Nishushe Dar Live. Sasa basi mwaka huu nitakuwa na kichaa wangu Stamina tutakavyoshuka njoo ujionee mwenyewe usije kusimuliwa,” alisema Roma.

Naye Stamina alisema, Dar Live mara yake ya mwisho kupiga shoo ilikuwa siku hiyohiyo na aliingia akiwa ndani ya Bajaj jukwaani hivyo mashabiki wategemee kitu cha tofauti mwaka huu.

“Sina maneno mengi, maneno siku zote huwa jukwaani, usikose mtu wangu!” alisema Stamina kwa kifupi. Kwa upande wake Maua Sama anayetamba na Wimbo wa Iokote alisema; “Kwa mara ya kwanza nitaidondosha Iokote ndani ya Dar Live hivyo usikose kuja kunishuhudia nikikinukisha.”

Stori: Mwandishi Wetu

 

Loading...

Toa comment