TAKRIBAN wanafunzi 52,000 wamefanya mitihani yao ya mwisho huku shule na vyuo vikiwa vinaendelea kufungwa ili kuepusha maambukizi ya #COVID19.
Wanafunzi hao walipimwa joto la mwili kabla ya kuingia kwenye mtihani huo ambao ni muhimu katika mfumo wa elimu wa Hong Kong, China.
Mitihani hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa muda mrefu, ilianza jana (Ijumaa) wakati janga la virusi vya corona likiwa limepamba moto ambapo wanafunzi zaidi ya sita hawakuweza kuifanya kutokana na kuwa na homa na magonjwa mengine.
Kwa mujibu wa mamlaka ya jiji hilo, wanafunzi 300 wengine walijiondoa katika mitihani hiyo kutokana kuugua au kuwa nje ya jiji hilo.
Kulikuwa na watahiniwa 52,000 waliokuwa wakitegemewa kuanza mitihani yao ya Diploma ya Elimu ya Sekondari, Machi 27 mwaka huu.
Hata hivyo, mitihani hiyo ilisogezwa mbele kutokana na janga la ugonjwa huo.





