Licha ya Kudai Kumrudia Mungu, Sabby Aendelea ‘kujirusha’


Imewekwa na on April 20th, 2017 , 01:38:06pm

Licha ya Kudai Kumrudia Mungu, Sabby Aendelea ‘kujirusha’

Na MAYASA MARIWATA| GAZETI LA AMANI| HABARI

MSANII wa Bongo Fleva, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ambaye siku chache zilizopita alitangaza kustaafu sanaa na kuamua kumrudia Mungu, ameon-ekana kulegalega msimamo wake huo baada ya kuonekana kwenye kumbi za starehe akila bata.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na bishosti huyo, kitendo cha Sabby kusema kuwa ameamua kuacha sanaa na kumrudia Mungu, yeye hakubaliani nacho kwani mara kadhaa amekuwa akimuona viwanja mbalimbali vya starehe akijiachia, jambo ambalo mtu aliyemrudia Mungu hawezi kulifanya.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo paparazi wetu alimvutia waya Sabby aliyekuwa na haya ya kusema: “Mmh! Sina hata la kujitetea, ukweli nimeamua nimrudie Mungu, lakini haya mambo ya starehe najitahidi kuacha kidogokidogo, hadi pale nitakapoweza kuacha kabisa kwenda klabu na upuuzi mwingine.”

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Be the first to comment on "Licha ya Kudai Kumrudia Mungu, Sabby Aendelea ‘kujirusha’"

Leave a comment