The House of Favourite Newspapers

Ligi iishe Salama Timu Zijipange Msimu Ujao

0
Kikosi cha timu ya Yanga.

LIGI Kuu Bara inafikia tamati leo kwa timu zote 16 kucheza mechi zao za mwisho, nyingine itakuwa bingwa na tatu za chini zitashuka daraja kuzipa nafasi klabu zilizofanya vizuri katika Ligi Daraja la Kwanza.

Tofauti na msimu uliopita, msimu huu wa 2016/17 tumeona mambo mengi ikiwemo ligi kuwa ngumu na kupata matokeo yasiyotabirika kiasi cha kuongeza msisimko tofauti na siku za nyuma.

Kikosi cha timu ya Kagera.

Ujio wa timu kama Mbao FC ulileta chachu mpya kiasi cha kuzitetemesha timu vigogo vya ligi hiyo lakini hadi leo kikosi hicho kipo katika hatari ya kushuka daraja.

Simba awali ilionekana kuwa katika nafasi ya kutwaa ubingwa lakini ghafla kibao kikageuka na Yanga ikashika nafasi hadi leo ina nafasi kubwa ya kuwa bingwa.

Ni kipindi cha timu zilizokosa ubingwa, kunusurika kushuka daraja hata zile zilizoshuka kuketi na kujiuliza kipi kiliwasibu hadi kuwa katika nafasi walizopo. Tunaomba mechi za leo ziishe kwa amani na timu zijipange kwa msimu ujao.

Kila la kheri Ligi Kuu Bara.

 

Leave A Reply