LIGI KUU YA WANAWAKE NI YANGA PRINCES NA SIMBA QUEENS JUMAPILI

LIGI Kuu ya Wanawake inaendelea Jumapili Januari 13, 2019 kwa michezo mitatu ambapo Yanga Princes itavaana na Simba Queens Uwanja wa Karume jijini Dar es Salamam jijini Dar es Salaam.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia yao ya utani wa jadi wa timu hizi mbili zinapokutana, msimu huu ni maraya kwanza kwao kwa kuwa Yanga Princess imepanda daraja msimu huu.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Cliford Ndimbo amesema ni wakati wa mashabiki kujitokeza kwa wingi kuona ladha ya ligi hiyo ambayo ni tofauti na msimu uliopita.

Simba Queens wamecheza michezo minne wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 10 huku Yanga wamecheza michezo minne wamekusanya pointi sita huku kinara akiwa ni JKT Queens mwenye pointi 12 baada ya kucheza michezo minne.

2. JKT Queens itavaana na Alliance Girls mchezo ambao utapigwa katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza,

3. Baobab Queens itavaana na Mlandizi Queens Uwanja wa Jamuhuri Dodoma.

 

Loading...

Toa comment