
Ligi ya Beach Soccer Imeendelea Tena Katika Viwanja vya Coco Beach
Beach Soccer mambo ni moto
LIGI ya Beach Soccer imeendelea katika viwanja vya Coco Beach ambapo mechi za makundi mawili A na B zilichezwa.
Ulianza mchezo wa Kundi A kati ya Ilala v PCM ambapo baada ya mchezo kukamilika ubao ulisoma Ilala 7-7 PCM na mshindi alipatikana kwa penalti na ni Ilala ilishinda penalti 5-3 PCM.
Mchezo wa kundi B ulianza ule wa Sayari dhidi Mburahati na Sayari ilipata mabao 3-4 Mburahati.
Mashindano yanaendelea kushika kazi katika viwanja vya Coco Beach
Katika mchezo wa pili wa kundi B katika Ligi ya Beach Soccer inayodhamiwani na Global Online uliwakutanisha Kijitonyama v Mshikamano FC na ulikamilika kwa Kijitonyama kushinda mabao 9-3.
Mchezo wa mwisho ulikuwa kati ya Kisa FC 2-4 Mburahati

