The House of Favourite Newspapers

Ligi ya Ilemela kuchezeshwa kama UEFA

0

Ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Imelela jijini Mwanza imefika hatua ya nusu fainali ambapo hatua hiyo inatarajia kuendelea julai 3, mwaka huu kwenye uwanja wa sabasaba jijini hapa kwa timu nne kuonyeshana ubabe katika michuano hiyo.

Akizungumza na Globalpublishers Katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Ilemela Almas Mosh amesema ligi ya msimu huu ambayo ilianza kwa kushirikisha jumla ya timu nane ilikua na ushindani mkubwa kiasi cha kupata timu nne ambazo sasa zitacheza hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo ambayo kwa msimu huu imeshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 20 kama ambavyo shirikisho la soka hapa nchini TFF walizitaka wilaya zote za wilaya hapa nchini kushirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 20 jambo ambalo Ilemela wamelitekeleza.

Timu ambazo zimefika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Ilemela ni pamoja na Kiseke Unitd, First Born,Bilo FC pamoja na Jonas FC ambapo mashindano hayo hatua ya nusu fainali itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ambapo faida ya bao la ugenini imefungwa na sasa itachezeshwa kwa kufuata mtindo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA.

Leave A Reply