LIGI KUU YA ITALIA LIGI YA WABISHI
LIGI Kuu ya Italia imeendelea kushika kasi na Juventus wameonekana kuwa moto sana kwa sasa wakiwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwa msimu huu.
Hii ni kati ya timu inayopewa nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri kwenye ligi hiyo, mwanzoni walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kupata upinzani kutoka kwa Napoli, lakini sasa mambo ni tofauti wakiwa kileleni kwa tofauti ya pointi tisa na wapo nyuma kwa mchezo mmoja.
Ligi hiyo imekuwa na mambo mengi ambayo mashabiki wanatakiwa kuyafahamu na kuelewa kuwa hii ni kati ya ligi kubwa zaidi Ulaya kwa sasa:
KINARA
Kinara wa ligi hii ni Juventus ambao wanaongoza kwa tofauti ya pointi tisa wakiwa wamecheza michezo 20, wameshinda 18 na kutoka sare michezo miwili wakiwa hawajafungwa mchezo wowote. Juventus ndiyo timu ya pili kwenye ligi kuu tano za Ulaya kwa sasa ambayo msimu mzima haijapoteza mchezo wowote ukiacha PSG ya Ligi Kuu ya Ufaransa.
MABAO Pamoja na Juventus kuongoza Ligi Kuu Italia, na kwenye suala la kufunga mabao wanaongoza wakiwa na mabao 41 Napoli ambao wamecheza michezo 20 wako nafasi ya pili na mabao 39. K w a upande wa kuf u n gwa, J u vent u s ndiyo i m efung w a m a b a o macha c h e baada ya kuruhusu n y a v u zake kutikiswa mara 11 tu ikiwa inafuatiwa na Inter Milan ambao wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa wamefungwa mabao 14 msimu huu hadi sasa.
KINARA WA MABAO
Cristiano Ronaldo amekaa kileleni kwenye chati ya ufungaji baada ya kuwania nafasi hiyo kwa muda mrefu akiwa na mabao 14. Staa huyo wa Juventus amecheza mechi zote za Juve msimu huu, akiwa pia ametoa pasi tano za mabao hadi sasa, anafuatiwa na Fabio Quagliarella wa kikosi cha Sampdoria ambaye naye amefunga mabao 14 na pasi tano za mabao.
Nafasi ya tatu kwenye ufungaji wa timu hiyo inashikwa na Duván Zapata wa kikosi cha Atalanta, akiwa na mabao 14 lakini pasi zake za mabao ni tatu, hawa ndiyo wanapambana kuhakikisha kuwa mmoja wao anatwaa tuzo ya ufungaji bora msimu huu.
ASISTI Ligi hii imekuwa ikiendelea kuonyesha kuna mastaa wengi wakubwa na kinara wa kupiga pasi za mabao huko anatoka AC Milan ambayo ipo nafasi ya sita, huyu anaitwa Suso, akiwa amepiga pasi nane za mabao hadi sasa.
Huyu anafuatiwa na fundi mwingine Dries Mertens ambaye anakipiga kwenye kikosi cha wahuni Napoli akiwa na pasi saba. Wengine wanaofuata ni Alejandro Gomez wa Atalanta ambaye ana pasi tano, Cengiz Under wa Roma mwenye tano sawa na Cristiano Ronaldo wa Juventus na Fabio Quagliarella wa Sampdoria.
Comments are closed.