Lijualikali: Chadema Mjipange, TAKUKURU Wana Ushahidi Wote

MBUNGE wa Kilombero , Peter Lijualikali, amefika katika ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa (Takukuru) Makao Makuu Dodoma leo Juni 11, 2020, kwa ajili ya kuhojiwa juu ya malalamiko ya matumizi ya fedha za michango waliyokuwa wakikatwa kila mwezi.
Lijualikali ambaye alikuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya kutimuliwa na kuomba kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewaonya wabunge wenzake wa Chadema ambao bado hawajahojiwa na Takukuru kutoa taarifa za kweli watakapokuwa wanafanyiwa mahojiano kwani taasisi hiyo imejipanga na kwamba wana taarifa zote.
View this post on Instagram

