The House of Favourite Newspapers

Lil Wayne Ampa Drake Zawadi Ya Bei Mbaya – (PICHA)

 

RAPA Lil Wayne ameonyesha heshima na upendo kwa msanii Drake baada ya kumnunulia cheni ya bei mbaya.

 

Mtengenezaji wa cheni hiyo ameiweka katika akaunti yake ya instagram na kuandika ni oda ya Lil Wayne ambayo ni zawadi kwa rapa wake, Drake.

 

 

Pindi Weezy alipomsaini Drake  kwenye lebo ya ‘Young Money’,  wawili hao walionekana kuwa na ukaribu mkubwa sana tofauti na ukaribu wa kibiashara.

 

Vilevile ikumbukwe kwamba Julai 25, 2017 Drake alionyesha tattoo ya Lil Wayne aliyomchora kwenye mkono wa kushoto chini ya bega.

 

Haijafahamika bado zawadi hiyo imegharimu kiasi.

Comments are closed.