The House of Favourite Newspapers

Linah Aanika Idadi ya Wanaume Aliyotembea Nao

 

MWANADADA anayekimbiza kwenye muziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga amefunguka na kutaja idadi ya wanaume ambao ametembea nao na kufaidi penzi lake tangu awe maarufu.

 

“Kwa haraka haraka nishatoka kimapenzi na wanaume watano hivi toka hivi watu wamenifahamu kama Linah, sina idadi kubwa sana, japo siwezi kuwakumbuka wote wengine nimeshawasahau kabisa. Kuna watu wana idadi kubwa ya watu wametembea nao sema tu ni kwa sababu si wasanii,“ amesema Linah.

Linah amesema hayo wakati akifanya mahojiano yake na EATV kwenye kipindi cha Kikaangoni na kuongeza kuwa idadi hiyo ya wanaume ni baada ya kupata jina, lakini aliyowahi kutoka nao kimapenzi kipindi cha nyuma kabla ya umaarufu hawakumbuki ila ni kati ya 10 au 15.

 

Linah amesema anavutiwa kimahaba na wanaume wenye rangi ya ngozi nyeusi tofauti na wengine wanavyochagua watu wa kuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi.

 

“Mimi napenda wanaume weusi, warefu si unajua mimi mfupi (shoti), sipendi wanaume weupe japo nishawahi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume mweupe ambae ni Naga aliyekuwa ananisimamia katika kazi zangu hata ile ya ‘project’ yangu ya Ole Temba”, amesema Linah.

 

Aidha, Linah amesema rangi yake hajichubui lakini aknaoga vizuri hana stress zozote, na anaweza kununua mafuta mazuri ya kupaka tofauti na enzi zile alikuwa akipaka mafuta ya mgando.

Comments are closed.