LINAH ADAIWA KUJALADIA MAKALIO
MREMBO kutoka Bongo Flevani, Esterlina Sanga ‘Linah’ amekwaa skendo ya ‘kujaladia’ makalio baada ya kuonekana katika picha mpya akiwa amejaa zaidi eneo la nyuma. Wananzengo wa Instagram wamesema Linah waliyemzoea hayupo hivyo japo watu wake wa karibu wamemtetea kwa kusema si kweli bali Linah ndivyo alivyo kwa sasa.
“Watu tu hawajamuona Linah hivi karibuni, ndivyo alivyo, hajajaladia wala nini mtoto wa watu Mungu kamjalia,” alisema rafiki yake aliyeongea na Udambwi wa Insta. Alipotafutwa Linah mwenyewe simu yake iliita bila kupokelewa.
Comments are closed.