LINAH, BELLE9 KUKIWASHA IRINGA WASAFI FESTIVAL…

Linah

BAADA ya uzinduzi wa kutisha wa Wasafi Festival kufanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, leo (Ijumaa) moto utawaka ndani ya Uwanja wa Samora mkoani Iringa ambapo wakali wapya Linah pamoja na Belle9 wameongezwa kwenye listi. Akizungumza na Ijumaa, mratibu wa tamasha hilo, Ricardo Momo alisema; “Kwa Iringa tumeongeza wasanii wengine wapya ambao ni Belle9 na Linah, lakini kuna baadhi ya wasanii hawatakuwepo ambao ni Kisamaki, Ibra Nation, Katrina na Navy Kenzo, tunaenda sasa kuanza safari ya makamuzi yetu naomba mashabiki wote wa burudani waje kuona ni namna gani wasanii wetu wamejipanga,” alisema Momo.

Wasanii kwa ujumla watakaokinukisha Iringa ukiachilia waliotajwa hapo juu ni One Incredible, Stereo na Nikki Mbishi hawa kwa upande wa Hip Hop, wengine ni Khadija Kopa, Chin Bees, Moko, Young Killer, Dudu Baya au Konki Master.

“Baada ya Iringa, mapinduzi ya burudani yataendelea tena kutokea siku ya Jumapili ya Desemba 2, mwaka huu ambapo tutakuwa tukiumiza nyasi za Uwanja wa Jamhuri pale mkoani Morogoro, kwani pale pia tunatarajia kuongeza wasanii huku tukipunguza ambao watakuwa na siku chache tu wametumbuiza pale,” alisema Momo.

Watakaongezeka kwa Morogoro ni Linah, Afande Sele, Belle9 na Navy Kenzo lakini kwa upande wa Bongo Movie watakuwepo Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper na Steve Nyerere.

Stori: Musa Mateja

Toa comment