The House of Favourite Newspapers

Linah hata kama unapiga ‘masanga’, piga kwa stepu!

0

linaKWAKO ndege mnana, Esterlina Sanga ‘Linah’, uhali gani mtoto mwenye sauti ya kipekee uliyetokea kwenye Jumba la Vipaji Tanzania (THT)? Shughuli zinakwendaje?
Kama muungwana, nimekukumbuka leo kwa barua. Kitambo kidogo hatujaonana.

imeona bora nikuandikie ili kufikisha kile ambacho kipo ndani ya nafsi yangu.
Ukitaka kujua hali yangu, mimi sijambo. Namshukuru Mungu maisha yanasonga kama kawa, huku nikiendelea kupambana katika shughuli za kila siku ili mkono uende kinywani, si unajua mjini hapa!

Dhumuni la barua hii kwanza ni kukusalimia. Baada ya salamu, nataka nikushauri katika eneo la mambo yetu yale ya usiku. Pombe bwana inahitaji akili ya ziada kujikontroo. Kilichotokea juzikati katika pati ya msanii mwenzenu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kilikuwa si cha kistaarabu.

Ulionesha dhahiri kwamba ulichangamka. Kitendo cha wewe kufunua nguo hadi kubaki na ile ya ndani, kilionesha ni jinsi gani staha yako imechepuka. Kwamba ulionekana si wewe bali ni akili za ziada zilisababisha ufanye yale uliyoyafanya.

Matokeo yake hata zile picha zilipowekwa kwenye mitandao na vyombo vya habari, ilikuwa aibu kwako. Watu wanapenda muziki wako, hawategemei kwamba unaweza kufikia hali ile wakati wewe ni mtu unayeheshimika.

Hata wale wasanii wachanga ambao wanategemea wajifunze kutoka kwako, unafikiri kwa mwendo ule watajifunza nini. Unataka kuwafanya wazazi wao nao waamini muziki ni kujitangaza kwa staili ile uliyofanya?

Kiroho safi kabisa nakushauri, kama siku ile maji yalizidi unga basi inabidi ujitazame upya katika eneo la ‘kilaji’. Ujue kabisa kiwango chako kikoje? Ili angalau unapokuwa kwenye hafla kama hizo uwe unajimudu.

Kitendo cha wewe kusaula kiasi kile hakipaswi kufanywa na mtu wa aina yako ambaye una wadogo zako wengi pale THT na nchini kote ambao wanafuata nyayo zako. Wanatamani siku moja nao wawe kama wewe.

Nimekushauri kama kaka yako lakini pia shabiki wako. Napenda kuona unakua, napenda kuona mafanikio yako ila ninapoona unajiingiza katika skendo za aina hii unafanya nikufikirie tofauti wakati mimi naamini wewe ni mtu makini.
Ni mtu ambaye umetoa mchango wako kwenye gemu hususan katika kizazi cha mabinti wachache waimbaji Tanzania.

Kwa hayo machache nina imani utakuwa umenielewa na utafanyia kazi ushauri wangu, nikutakie safari njema katika mwaka huu wa 2016. Uwe wa mafanikio kwako!
Ni mimi kaka yako,

………………….
Erick Evarist

Leave A Reply