Lindi: Aliyemuua Mkewe Ahukumiwa Kusafisha Hospitali
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Luyaya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, Atanasi Kijombo, adhabu ya kufanya usafi kwenye mazingira yanayozunguka Hospitali ya Wilaya ya Kilwa kwa miezi 12, baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Mkewe Hadija Mambo bila kukusudia.
Kijombo alimuua Mkewe bila kukusudia baada ya kushikwa na hasira pale alipomkuta Mke wake huyo akifanya mapenzi na Mwanaume mwingine.
Comments are closed.