The House of Favourite Newspapers

Lissu Aahidi Bima za Afya Nchi Nzima

0

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu, ameahidi kuwa iwapo atachagukliwa kuwa rais atahakikisha kila Mtanzania anapata bima ya afya ili kuweza kumudu gharama za huduma za afya.

 

Lissu ameeleza hayo jana Septemba 4, 2020, akiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho mkoa wa Tabora.

 

“Serikali yetu, serikali ya CHADEMA itahakikisha kwamba, kila Mtanzania na kila mkazi wa Tanzania, anapata bima ya afya,” alisema Lissu.

 

“Ninafahamu, kwa sababu nimepita katika hospitali nilizosema kwa miaka mitano, ninafahamu kwamba bima ya afya ni gharama, ukiweka utaratibu wa kila mtu kuwa na bima ya afya, ile gharama ambayo mtalipa kwa mwaka itakuwa ndogo sana,” aliongeza Lissu.

Leave A Reply