The House of Favourite Newspapers

Lissu Ashinda Nafasi ya Uenyekiti Chadema, Heche Makamu Mwenyekiti Bara – Video

Tundu Lissu ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema baada ya kupata kura 513 kati ya kura 996, sawa na asilimia 51.5.

Freeman Mbowe yeye amepata kura 482 kati ya kura 996, sawa na asilimia 48.3.

Odero Charles yeye amepata kura 1, sawa na asilimia 0.1.

John Heche ametangazwa rasmi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bara baada ya kupata kura 577 kati ya kura 998, sawa na asilimia 57.

Akitangaza matokeo hayo, mmoja kati ya wasimamizi wa uchaguzi huo, Profesa Raymond Mosha, amesema Ezekiel Wenje amepata kura 372, sawa na asilimia 37 huku Mathayo Gekul akipata kura 49, sawa na asilimia 5.

Heche alikuwa upande wa Tundu Lissu aliyemwangusha Freeman Mbowe katika nafasi ya uenyekiti.

Matokeo hayo yametangazwa na mmoja kati ya wasimamizi wa uchaguzi huo, Profesa Raymond Mosha katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.