The House of Favourite Newspapers

Lissu, Kibatala Wapinga Ushahidi wa Bangi Kesi ya Wema (VIDEO)

0
Kushoto ni Wakili Peter Kibatala na Wema Sepetu (mwenye gauni jeupe), akiwasili mahakamani hapo.

 

USHAHIDI unaoendelea kutolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam dhidi ya msanii Wema Sepetu, umezidi kupingwa na mawakili wanaomtetea akiwemo Tundu Lissu na Peter Kibatala.

Ofisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo alileta vithibitisho anavyotuhumiwa kukutwa navyo Wema Sepetu na watuhumiwa wengine wawili ambavyo ni misokoto miwili ya bangi ambayo ilikuwa imefungwa katika bahasha.

 

Wema akiwa na mama yake.

 

Upande wa utetezi ukiongozwa na Tundu Lissu uliukataa ushahidi huo kwa madai kwamba wakili wa serikali aliiambia mahakama kuwa ushahidi huo ulikuwepo lakini hakuiambia mahakama kuwa ulikuwa umefungwa ndani ya bahasha.

Lakini hoja ya wakili wa serikali kwamba bahasha ndiyo ushahidi aliiondoa baada ya kutakiwa kueleza kilichokuwemo ndani ya bahasha ili kitambulike kama ushahidi.

Wema akiondoka mahakamani hapo.

Baada ya kuondoa hoja hiyo, Hakimu wa Mahakama hiyo Thomas Simba alimwamuru mtoa ushahidi kuifungua bahasha, japo upande wa utetezi uliukataa ushahidi huo kwa madai kuwa ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na vielelezo vingine ambavyo mtoa ushahidi hakuvieleza awali, kikiwemo kitu kilichodhaniwa kuwa karatasi nyekundu.

Baada ya kusikiliza hoja hizo hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18 ili aweze kutoa ufafanuzi juu ya ushahidi huo.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

==

VIDEO: Lissu, Kibatala Wapinga Ushahidi wa Bangi Kesi ya Wema

Leave A Reply