Kartra

Litombo Aipa Kiburi Yanga SC

UONGOZI wa Yanga, umetamba kuwa umelamba dume kwa beki wa kati mpya wa timu hiyo, Mkongomani, Yannick Bangala Litombo kutokana na kumudu kucheza nafasi tatu ndani ya uwanja.

 

Beki huyo muda wowote atatambulishwa na uongozi wa Yanga mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

Kutua kwa Litombo kutaimarisha safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa inaongozwa na Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema sababu ya kufanikisha haraka usajili wa Litombo ni uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi tatu.

 

Mwakalebela alisema Litombo anamudu kucheza nafasi ya beki wa kati namba 5, pembeni namba 2 na kiungo mkabaji namba 6.

 

“Litombo atatumika na kocha kutokana na mahitaji yake, hiyo ni kutokana na kumudu kucheza nafasi tatu tofauti ndani ya uwanja. Hivyo tunajivunia usajili huo ambao muda wowote utatangazwa baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

Hiyo ndiyo inayotupa jeuri ya sisi kukubali kucheza na watani wetu Simba huku Morocco katika mchezo wa kirafiki kabla ya kuja kucheza nao katika Ngao ya Jamii huko nyumbani, msimu ujao tunataka kuchukua vikombe vyote tutakavyoshindania,” alisema Mwakalebela.

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam


Toa comment