The House of Favourite Newspapers
gunners X

Simba Yawatungua AS Vita Kinshasa, Yaongoza Kundi

0

WAWAKILISHI wa kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wakiwa hatua ya makundi jana walianza kwa kasi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vigogo wa DR Congo, AS Vita.

 

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Des Martyrs, jijini Kinshasa ulikuwa na ushindani mkubwa na Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes iliwalazimisha wenyeji wao AS Vita kwenda mapumziko wakiwa suluhu.

Kumbuka mchezo uliopita wa 2018/19 kwenye michuano hiyo katika hatua hiyohiyo ya makundi, ikiwa uwanjani hapo Simba ilichapwa mabao 5-0 na As Vita hivyo sasa vijana wa Msimbazi wameweka rekodi ya kushinda ugenini dhidi ya Vita katika misimu ya karibuni.

 

Iliwachukua Simba dakika 60 kuandika bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Chris Mugalu kwa mkwaju makini wa penalti baada ya kumchambua kipa wa AS Vita ambaye alipotezwa akiwa kwenye lango.

Penalti hiyo ilisababishwa na kiungo machachari wa Simba, Luis Miquissone ambaye alimnawisha mpira mchezaji wa AS Vita ndani ya 18 na Mugalu hakufanya ajizi aliuzamisha ndani ya nyavu.

 

Shukrani kwa kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula ambaye alifanya kazi kubwa ya kuokoa hatari za nyota wa AS Vita ambao walikuwa wakiliandama lango lake kipindi cha kwanza na kipindi cha pili.Dakika ya 9, dakika ya 35, 41 na 78 aliokoa hatari ambazo zilikuwa zikienda langoni mwao ambapo AS Vita walikuwa wakimtumia Fiston Mayele na Juma Shaban ambao waliisumbua safu ya ulinzi ya Simba.

Thadeo Lwanga na Mzamiru Yassin waliweza kucheza kwa maelewano makubwa eneo la kati kwa kukata umeme ndani ya uwanja.

 

Huku eneo la ulinzi, Pascal Wawa na Joash Onyango wakicheza kwa umakini licha ya makosa ambayo yalikuwa yanafanywa katika kuokoa mipira.Kiungo wa zamani wa Yanga, Papy Tshishimbi alitolewa uwanjani dakika ya 56 baada ya kushindwa kuendana na kasi ya Lwanga ambaye alikichafua eneo la kati.

Mugalu alitumia dakika 79 na kumuachia nafasi Meddie Kagere ambaye aliweza kutengeneza nafasi dakika ya 81 na kipa wa AS Vita alitoka kufuata mpira ila aliukosa na mabeki wa AS Vita waliweza kuokoa hatari hiyo.

 

Kadi tatu za njano zilionyeshwa kwenye mchezo wa jana, Lwanga na Pascal Wawa walionyesha kwa upande wa Simba na kwa Vita alionyeshwa Vivien Koua.

Mchezo wa wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya AS VITA vs SIMBA SC unachezwa leo Februari 12, 2021, huko nchini DRC Congo.. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply