BREAKING​: Murtaza Mangungu Mwenyekiti Mpya Simba -Video

UPDATES: Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba ni Murtaza Mangungu baada ya kupata kura 802 (70.35%) akimshinda Juma Nkamia aliyepata kura 330 (28.95%).

Jumla ya kura zilizopigwa ni 1140 na kura 8 (0.7%) zimeharibika.

 LEO Jumapili, wanachama wa Simba SC watapata fursa ya kufanya uchaguzi mdogo wa mwenyekiti wa wanachama kuziba nafasi ya Swedi Mkwabi aliyejiuzulu Septemba, 2019.

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar, wagombea wawili ndiyo wanaowania nafasi hiyo ambao ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lihamwike, alisema: “Kuelekea uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa klabu ambaye atakuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi umekamilika, tumepitia hatua mbalimbali, ukiachana na uchaguzi, kesho (leo) kutakuwa na mkutano mkuu wa wanachama.“

Wagombea wawili ambao ni Murtaza Mangungu na Juma Nkamia ndiyo walikidhi vigezo, hawa ndiyo wanawania nafasi hii ambayo iliachwa na Swedi Mkwabi.“Niwakumbushe wanachama ambao hawajalipia kadi zao kutakuwa na utaratibu maalum wa kulipia, hivyo wanatakiwa kuwasili mapema ili kuepuka usumbufu,” alisema Lihamwike.

 

Mkutano huo unatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na kumalizika mapema ili kutoa fursa kwa wanachama wa Simba kwenda uwanjani kushuhudia mechi ya timu yao dhidi ya Azam

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Toa comment