The House of Favourite Newspapers

VIDEO + PICHAZ: Shuhudia Uzinduzi wa Movie Mpya ya Msanii Jacob Steven ‘JB ‘

0

Msanii wa Filamu za Bongo Movie, Jacob Steven maarufu kama JB leo Aprili 21, 2017 amezindua filamu yake mpya inayoitwa ‘Hadithi za Kumekucha’.

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi uliyopo kwenye Jengo la Quality Plaza, jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza wakati wa kuitambulisha filamu hiyo mpya,  waandaaji wa filamu hiyo walieleza kuwa filamu hiyo inazungumzia maisha halisi ya Mtanzania, hasa vijana ambao wamekuwa wakikataa kuishi vijijini.

Mbali na hivyoi hivyo, filamu hiyo imejikita katika kushauri vijana wajihusishe na kazi za kilimo hasa cha kisasa ambacho kinaweza kuwapa tija katika kupambana na umaskini.

JB akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu hiyo.

Kwa upande wake JB ameeleza kuwa, filamu hiyo ni ya kiwango cha juu ikilinganishwa na filamu nyingine ambazo ameshawahi kucheza ama kuziandaa kwani ni bora, ina uhalisia na hauwezi kuchoka kuitazama.

Mmoja waandaaji wa filamu hiyo akifafanua mambo kadha wa kadha kuhusu ‘Hadithi za Kumekucha’.

Akizungumzia mvutano uliyopo kuhusu kuzuia filamu za nje kuingizwa nchini, JB alisema kuwa wauzaji wa filamu za wamekuwa waki-download kisha wana-burn kuziuza kwa bei nafuu kuliko za Bongo Movie hivyo kufanya watazamaji wanunue z nje kwani zina bei ndogo huku akikiri kuwa filamu hizo za nje zina ubora zidi kuliko za ndani.

Mbali na hivyo, JB alitoa malalamiko yake akisema kuwa filamu hizo za kudownload zimekuwa zikiuzwa mitaani bila stika wala kulipiwa mapato TRA tofauti na Bongo Movie ambao wanaweka stika na kulipia mapato TRA ambapo jambo hilo amedai kuwa linawanyonya wasanii wa ndani.

 

Baadi ya washiriki kwenye movie hiyo wakiwa wamepozi.

Mmoja wa washiriki wa Filamu hiyo akizungumzi uhusika wake wakti wa uandaaji wa filamu hiyo.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.

PICHA ZOTE NA DENIS MTIMA | GLOBAL TV ONLINE

==========================

TAZAMA FULL VIDEO YA UZINDUZI WA FILAMU YA HADITHI ZA KUMEKUCHA

Leave A Reply