The House of Favourite Newspapers

KATIBU MKUU CCM: WANANCHI WAMETUELEWA – VIDEO

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema wananchi wamezidi kukiamini na kukielewa ndiyo maana kimekuwa kikiibuka na ushindi katika chaguzi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika huku baadhi ya viongozi kutoka vyama vya upinzani wakihamia CCM.

 

Hayo yamesemwa leo, Agosti 13, 2018, na Katibu Mkuu CCM Taifa, Dk. Bashiru Ally wakati akizungumza na wananchi akitoa tasmini ya uchaguzi mdogo uliofanyika jana Jumapili katika Jimbo la Buyungu na kata mbalimbali hapa nchini.

 

“Buyungu tulipata taabu kidogo kwa sababu mbunge wao aliyefariki (Kasuku Bilago) alikuwa anapendwa sana na wananchi, wapinzani waache kufanya porojo mitandaoni wakati hata site hawakuwepo.

 

“Tangu tuanze kuongoza taifa hili, hatukuwahi kuwa na kura ndogo. Zipo kata ambazo tangu mfumo wa vyama vingi uanze hakujawahi kushika madaraka lakini katika Uchaguzi huu wa marudio tumeweza kushinda tena kwa kishindo.

 

“Tunataka kuua siasa za kibinafsi, za nafsi moja na mtu mmoja, ndo maana Rais hapendi ubinafsi, tunataka kuua utaratibu wa siasa ndani ya nchi yetu. Nchi yetu iko salama kabisa na tuwe makini tunapozungumzia vyombo vya utendaji na tuache kuhoji kwa kuangalia tukio moja, amesema yako matukio ambayo kweli hayapaswi kuachwa,” amesema Dkt. Bashiru.

 

Comments are closed.