Moto Mkubwa Waibuka Kariakoo (Video)

Moto ukitekeleza ghorofa ya juu ya jengo hilo eneo la Kariakoo.

MOTO mkubwa umeibuka Kariakoo katika mitaa ya Livingstone na Aggrey na unaendelea kuteketeza maduka. Tayari vikosi vya zimamoto vipo eneo la tukio kupambana na moto huo unaoendelea kuteketeza jengo la ghorofa ambalo lina maduka katika ghorofa ya chini.

Moto huo ulianzia kwenye ghorofa ya kwanza katika jengo hilo lenye ghorofa mbili ambako kulikuwa na stoo ya vitu mbalimbali ambavyo vimeteketea kwa moto huo ambao moto huo ulielekea katika ghorofa ya juu.

Chanzo cha moto huo hadi tunakwenda mitamboni kilikuwa hakijajulikana.

Mmoja wa watu waliokuwa wakiishi katika ghorofa iliyoungua kwa moto (kushoto) akiwa analia.

Sehemu ya ghorofa ambapo moto ulianzia.

Vikosi vya zimamoto hivi sasa vinaendelea kukabiliana na moto huo ambapo upande mmoja wa ghorofa hiyo umezimwa.

Wingu la moshi likitoka sehemu moto ulipokuwapo.

Wakazi wa Dar es Salaam wakishuhudia moto huo.

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment