The House of Favourite Newspapers

CHADEMA Walia na JPM, Kesi ya MBOWE – Video

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, amewaomba wanachama wa Chadema na Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi Mahakama ya Kisutu kesho Desemba 6, 2018 kwa ajili ya kuwafariji Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, ambao watafikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza tena kesi inayowakabili.

 

“Wale watakaoshindwa kwenda Mahakamani muitumie siku hiyo kuwa pamoja nao kukumbuka kifo cha Akwilina kwenye uchaguzi ambacho ndio kimepelekea viongozi kubambikiwa kesi na mambo yanayohusu mabadiliko ya kimfumo katika uchaguzi katika nchi yetu.

 

“Mahakama ya rufaa ilishughulikia rufaa hii kwa haraka kabla ya kufungwa mikono na Serikali kwa matumizi mabaya ya mamlaka ya DPP kupeleka notisi, ilishaanza kushughulikia mapingamizi kwa hatua za haraka kwa sababu maamuzi yameshafanywa na Mahakama ya rufaa.

 

“Nimuombe msajali wa Mahakama kwa uharaka alioshughulikia shauri na tunashukuru kwa hatua hiyo waweze kukamilisha kiporo kilichobaki kilichopo kwenye mamlaka yao kukamilisha rekodi za rufaa ili Serikali isiwe na kisingizio cha kuendelea kuchelewesha shauri hili.

 

“Tayari tumeshachukua hatua za kiutawala kupitia kwa mawakili wetu kuiandikia barua Mahakama ili iweze kutumia mamlaka yake katika jambo hili ikiwezekana mamlaka ya kufanya mapitio kwenye faili lote lililopo Kisutu lililopo Mahakama Kuu linalohusiana na shauri hili.

 

“Maamuzi haya hayawezi kufanywa bila mamlaka za juu yao, sasa ili ionekane mamlaka za juu zinatenda haki ikiwemo Rais, Waziri wa Katiba na sheria,mwanasheria mkuu wa Serikali na DPP wanayo nafasi kabisa ya kuepusha Mahakama kupoteza muda na rasilimali za Mahakama.

 

“Na wewe kupeleka rufaa yenyewe na rufaa ikipelekwa kuna siku 60 ili kuichelewesha haki na tunaamini kwa sababu ni watu wale wale,wengine ndani ya Serikali wanasema ni maamuzi yao wenyewe wanasheria wa Serikali, mimi naamini maamuzi makubwa kama haya hayawezi.

 

“Sababu imedhihirika wazi kama ilivyokuwa kwenye kesi ya Godbless Lema huko nyuma ambapo katika kipindi hiki cha kuelekea likizo ya Mahakama upande wa Serikali unatumia vibaya mamlaka ya kupeleka notisi kuna muda wa siku 30.

 

“Masuala yote yalijitokeza kuanzia mwanzo hadi kufutwa kwa dhamana ya Freeman Mbowe na Ester Matiko, Mahakama ya rufaa itayafanyia mapitio na kutenda haki bila upendeleo wala kuingiliwa.

 

“Kwa misingi ya Katiba ya nchi ibara ya 107, inaweka kanuni kuu ya kutenda haki, (Principle of right objective), haki haitakiwi kuminywa kwa sababu za kiufundi, au sababu nyingine zozote ambazo zinaweza kuchelewesha haki

 

“Hakimu kukataa kujitoa, suala na Mawakili kujutoa kwa sababu ya haki kupindishwa pale Mahakamani , ikiwemo kusomewa maelezo ya awali (P.H.) kwa lazima bila ya hata kuwa na mawakili. Tunaamini ukitumika utaratibu huo ukitumika kuitisha faili lililopo Kisutu na Mahakama Kuu na kufanya mapitio tunaamini haitashguhulikiwa suala la kufutwa kwa dhamana lakini pia kuna masuala mengine kama masharti ya dhamana, kuripoti polisi kila Ijumaa.

 

“Tunapokwenda kesho Mahakamani, tunapenda kupeleka rai ya kutokuendelea na shauri au chochote kile wanachoweza kufanya wanaweza kuifuta hiyo kesi ,hata ile iliyopo Mahakama ya rufaa wanaweza kuindoa hiyo notisi iliyopo na shauri likarudi moja kwa moja Mahakama Kuu.

 

“Rais Magufuli, Waziri wa sheria, mwanasheria mkuu wa Serikali na DPP kama hawajawatuma hawa kufanya haya waliyoyafanya basi waingilie kati au tutaamini kauli aliyoitoa akiwa UDSM wa kutamani viongozi wa Chadema wawe magerezani ndo umekwenda kutekelezwa.

 

“Tunaiomba Mahakama ya rufaa popote pale ambapo ina kikao hivi sasa tunajua ina vikao vinaendelea nje ya Dar kabla Mahakama haijaenda likizo iziite pande zote ili shauri hili liweze kushughulikiwa kwa wakati,” amesema Mnyika.

VIDEO: TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.