The House of Favourite Newspapers

Polepole: Magufuli Anashinda Asilimia 85, Upinzani Watauza Madini – Video

0

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kwa tafiti walizofanya kutokana na kampeni za urais ambazo wamefanya mpaka sasa, iwapo uchaguzi ungefanyika leo, basi mgombea wao wa Urais, Dkt. John Pombe Magufuli angeibuka msindi kwa kupata asilimia 85 ya kura.

 

Polepole amesema hayo leo Ijumaa, Septemba 11, 2020 wakati akizungumza na wanahabari mkoani Geita na kutoa tathmini ya kampeni za CCM kwa siku 12 walizofanya na kutoa mwongozo kwa awamu ya pili ya kampeni za chama hicho.

 

“Mzee Jakaya Kikwete yupo Ukanda wa Kusini kule anavuruga, Mzee Pinda na Spika Job Ndugai nao wanaendelea. Muziki ni mzito mpaka sasa tunapozungumza kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni, tunafanya kampenzi za kisayansi.

 

“Kampeni kwa ujumla inakwenda vizuri sana, tumewafikia Watanzania na wametuelea mno, tumefanya tafiti za kisayansi kwa sababu tupo makini, kama kura zikipigwa sasa hizi Mheshimiwa Magufuli anaibuka na ushindi mnono wa asilimia 85, sasa hivi tunajazia tu kura.

 

“Kampeni za CCM 2020 tunazifanya kisayansi, tumegawanya viongozi waandamizi wa chama kwenye maeneo tofauti. Msafara mkuu unaongozwa na Dkt. Magufuli, msafara mwingine wa mgombea mwenza wa urais, Mheshimiwa Samia Suluhu, na mwingine unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya chama, Kassim Majaliwa, sisi hatutumii chopa.

 

“Tunatamani sana wenzetu watumie anga sisi tunachanja mbuga kijiji kwa kijiji, tumefuatilia madai yao kwamba wamezuiliwa tumebaini ni uongo, wanatengeneza chuki tu na upotoshaji, siku hiyo hawakuwa na ratiba ya kusafiri, mamlaka haikuwa na taarifa, umri wa rubani haukizi vigezo vya kurusha ndege Tanzania.

 

“Tangu Mheshimiwa Magufuli aingie madarakani hakujawa na mfumuko wa bei, tumefanya kazi nzuri mno, bidhaa haiongezeki, Mheshimiwa Magufuli amefuta kodi kwa wenye mishara midogo, hawa wanaosema ni wapotoshaji, tumelazimika kuwajibu, tunawaambia wasifanye siasa za hivyo.

 

“Ukisema kushuka kwa Diplomasia ni uongo, Mheshimiwa Magufuli ameingia tu madarakani akapewa uenyekiti wa EAC, ameendeleza mwendo wa kubana matumizi, miradi mikubwa imefanyika, ameacha alama, SADC amefanya mambo makubwa, MSD inapeleka dawa nchi zote za SADC, amefungua balozi nane mpya.

 

“Tunajenga viwanja vya ndege kila mkoa, Uwanja wa Mwanza ndiyo mkubwa zaidi ktk Ukanda wa Maziwa Makuu, ameupatia hadhi ya Kimataifa, vigezo vya kidunia ukiwa na Uwanja wa Kimataifa lazima uwe na uwanja wa kimkakati ikitokea hitilafu wanatua pale, Geita tumejenga Uwanja wa Mkoa na Uwanja wa Kimkakati (Strategic Aerodrome).

 

“Tunajenga viwanja vya ndege kila mkoa, Uwanja wa Mwanza ndiyo mkubwa zaidi ktk Ukanda wa Maziwa Makuu, ameupatia hadhi ya Kimataifa, vigezo vya kidunia ukiwa na Uwanja wa Kimataifa lazima uwe na uwanja wa kimkakati ikitokea hitilafu wanatua pale, Geita tumejenga Uwanja wa Mkoa na Uwanja wa Kimkakati (Strategic Aerodrome).

 

“Zamani wachimbaji wadogo walikuwa wakipata Kg 300 tu za dhahabu kwa mwaka, lakini sasa hivi wanapata zaidi ya Kg 6,000 kwa mwaka, Rais Magufuli alifanya maamuzi akapiga ukuta, wapinzani walitubeza, tunawaona akina Laizer wanavyopata mabilioni kutoka kwenye madini.

 

“Tumevuka nchi hii kwa sababu tuna hofu ya Mungu, dunia nzima imeshindwa Corona ni Tanzania pekee imesimama, mgombea wa Mbowe anasema akiingia madarakani ataacha kila mtu aamue kivyake, hatuwezi kuwa na nchi namna hiyo.

 

“Wanasema watatoa Bima ya Afya kwa wananchi wote, niwaulize; Unaweza kutoa Bima ya Afya wakati huna Hospitali? Unaweza kupanda mbegu katika shamba ambalo hujaliandaa? Sisi tumeongeza fedha ya dawa, vifaa tiba, miundombinu ya hospitali, tumeajiri madaktari.

 

“Wenzetu hawa wa upinzani wanazungumza mambo ya ajabu sana, wanasema watafuta kodi, vitambulisho vya machinga na mama lishe ili uwarudishe kupigwa na kunyang’anywa wali wao.

 

“Kwenye ilani yao, chama cha Mbowe wamesema hawatakusanaya kodi, watatumia madini yetu kuweka lehani halafu watakopa, wanapenda kwenda kukopa kwa kutumia mali ya Watanzania isiyohamishika, hawa ni walaghai wanataka kuuza nchi yetu, kazi imewashinda.

 

“Chama cha Mbowe wanasema wakiingia madarakani watachukua miradi yetu ya umeme, SGR, meli, ndege na nyingine ambayo inamilikiwa na Watanzania, wao wataibinafsisha tubaki na 50%, usione vyaelea, vimeundwa, hawa hawawajibiki Tanzania, wanawajibika kwingine.

 

“Tazama Ilani zao, mtu makini anaweza kusema mkinipa nchi nitawaletea ubwabwa? Mwingine anasema ‘Kazi na Bata’, dini gani inaruhusu starehe, imeandikwa ‘Utafanya kazi, kwa jasho lako utakula’, kuna bata hapo? Mwingine ‘Uhuru Haki Maendeleo’ hii sio kaulimbiu,” amesema Polepole.

 

Leave A Reply