The LiFe Club ‘Maisha Basement’ Kuzinduliwa Usiku wa Leo Ijumaa Dar
Klabu maarufu ya burudani ya The Life Club ‘Maisha Basement’ leo Ijumaa usiku inazinduliwa upya kwenye makao yake mapya yaliyohamishiwa katika ukumbi Mwenge Old Cinemax Century jijini Dar es Salaam. Zamani Klabu hiyo ilikuwa na maskani yake Makumbusho katika jengo la Milenium Tower.
Meneja wa Burudani wa The Life Club, Hemed Kavu ‘HK’ ameiambia Global TV Online leo Ijumaa kuwa wamejiandaa kutoa burudani ya aina yake na katika uzinduzi huo wamealikwa mastaa mbalimbali wa Bongo Fleva na wasanii wa muvi. Kiingilio kitakuwa Tsh 10,000/- kawaida na 20,000/- kwa VIP.
Uzinduzi huo unaanza saa tatu usiku amewaomba wapenda burudani kufika Mwenge Old Cinemax Century kujionea Klabu namba moja Tanzania kwa ubora wa kila kitu.
Pia ameongeza kuwa watakuwa wanatoa burudani kuanzia siku ya Jumanne mpaka Jumapili na wameweka mambo mengi ya kisasa ambayo mashabiki hawatajutia.
Comments are closed.