Dkt. Mpango Aapishwa Kuwa Makamu wa Rais – Video

Makamu wa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Philip Isdor Mpango ameapishwa kuwa Makamu wa Rais mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahimu Juma, leo Ikulu Chamwino jijini Dodoma.Uapisho huo umeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza baada kuapishwa, Dkt. Mpango amesema; “Mheshimiwa Rais mimi sikuota wala sikutarajia kwamba siku moja mimi mtoto wa masikini kutoka kwetu kule Buhigwe ningepata nafasi kutumikia taifa katika nafasi ya Makamu wa Rais.

“Nitakuwa mzalendo wa kweli kwa mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Rais kwa sisi wakristo kesho ndio tunaanza Juma Kuu, kuna mtu anaitwa Yuda ndio alimsaliti Yesu, mheshimiwa Rais mimi sitakuwa kama huyo Yuda.Nitatekeleza kwa bidii na weledi majukumu yote utakavyoniagiza.
“Niko tayari kuchapa kazi, nitume mchana na usiku na hususan kuhakikisha ahadi za Ilani ya CCM ya mwaka ya 2020 tunazitekeleza,” amesema Dkt. Mpango.

