KUFUATIA tukio la Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo na kufyatua risasi ambazo hata hivyo hazikumpata baada ya kufanikiwa kukimbia na mkewe, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo la kutisha.