The House of Favourite Newspapers
gunners X

HOTUBA ya JPM Akizindua Ujenzi wa Barabara Mtumba – Video

0

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Alhamisi, Juni 11, 2020 ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya lami ya Mtumba jijini Dodoma.

 

“Kabla sijaanza hotuba yangu nawaomba tutumie muda huu mfupi kumkumbuka Rais Nkurunziza wa Burundi na roho za marehemu waliotutoka leo zaidi ya 8 kwenye ajali ya Hiace kule Mwanza.

 

“Dodoma kweli imependeza na kila mmoja sasa anatamani kuja. Wanawake walikuwa weusi sasa ni weupe wengi, watani zangu Wagogo sasa wamebadilika.

“Nakumbuka hata niliposema tutahamia Dodoma ndani ya miaka mitano, wapo waliosema hizi ni ndoto za mchana, mimi huwa sioti mchana, huwa naota usiku tu. Kwa hiyo hata nikitoka mimi akaja Rais mwingine hatohama, atakaa hapa hapa Ikulu ya Dodoma, hili ni agizo.”

“Tumeshapata fedha Bilioni 500 za kujenga Uwanja wa Ndege mkubwa kama Dar es Salaam, ndege zitakuwa zinatua moja kwa moja kutoka Ulaya. Watani zangu Wagogo wale mbuzi wetu tunaotembeaga nao usiku tuwatoe kwenye uwanja wanaweza kuleta ajali.

“Dodoma ni mji unaokua vizuri, kuna miradi mikubwa inategemewa kujengwa ikiwemo ujenzi wa barabara ya mzunguko ya njia nne yenye urefu wa KM 110 zitakazogharimu zaidi ya TZS Bil. 600 na ujenzi wa Uwanja wa Ndege mkubwa utakaogharimu TZS Bil. 500.

“Tunamshukuru sana Mungu kwa kutuepusha na ugonjwa wa Corona, mambo yanaenda vizuri na tusidharau dawa za kienyeji uchawi tu ndiyo mbaya. Nimetoa maelekezo kwenye Wizara ya Afya, kile kitengo cha madawa ya asili kiendelezwe

“Tujipongeze sisi Watanzania kwamba yale tuliyoyapanga yamewezekana, leo ninapozungumza tumepata fedha za msamaha wa kodi kutoka kwa Bodi ya Wakurugenzi ya IMF, Dola Milioni 14.3 kwa sababu tulipambana vizuri sana na COVID-19.

“Nimepanga leo nitamuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa IMF kwa niaba ya Watanzania kuwapongeza kwamba wametambua juhudi na fedha hizi tutazitumia pia kupambana na Corona na kuzishughulikia kwenye maendeleo mengine ambayo yatatusaidia Corona isije tena nchini mwetu.

“Fedha hizi za msamaha wa kodi tutazitumia pia kupambana na Corona na maendeleo mengine ambayo yatatusaidia Corona isije tena. Ukishatengeneza barabara nzuri watu wakatembea haraka, yule mdudu hawezi kumsogelea mtu anayetembea,” amesema Magufuli.

 

Leave A Reply