The House of Favourite Newspapers

MAKONDA ATOA KIBALI KWA WASANII KUREKODI MOVIE ENEO LOLOTE  KUTANGAZA UTALII

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumzia wasanii namna wanavyoweza kutangaza utalii uliopo ndani ya mkoa wake.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  amepiga marufuku baadhi ya watendaji wanaozuia wasanii kurekodi Video za nyimbo zao kwenye mandhari (location) mbalimbali za jiji lake  na hivyo kupelekea kurudisha nyuma ukuaji wa utalii.

 

“Haiwezekani msanii akitaka kurekodi Video au Movie kwenye mitaro ya maji machafu ambayo inatoa taswira mbaya kwa jiji letu hasumbuliwi vibali lakini akirekodi kwenye hoteli, majengo marefu, fukwe au kwenye mazingira mazuri anasumbuliwa kwamba awe na kibali.

 

“kuanzia sasa wasanii mtarekodi sehemu yoyote mnayotaka isipokuwa sehemu ambayo ni maalumu kama vile Ikulu, mahakamani, maeneo ya jeshi na vituo vya polisi ambapo panahitaji vibali maalumu,” alisema Makonda.

 

Aliongeza kwamba lengo kubwa ni kuona wasanii wanapewa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya mkoa wake kupitia kazi za sana wanazozifanya.

 

 

 

Comments are closed.