The House of Favourite Newspapers

Hotuba ya Rais Magufuli Kilele cha Miaka 50 Ya BAKWATA – Video

Leo Disemba 18, 2018 Kumefanyika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Waislamu nchini BAKWATA ambapo katika sherehe hizo Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Makamu wa Rais pamoja na waziri mkuu.

 

Akihutubia katika hafla hiyo, Magufuli amesema;

“Serikali imefanya maendeleo makubwa kwa muda mfupi, watu wanajiuliza pesa tumetoa wapi, jibu ni kwamba tumewabana Mafisadi na kusimamia vyema rasilimali za Taifa letu lenye utajiri, lakini inasikitisha linaitwa Taifa maskini. Tumeamua kununua ndege mpya, nitashangaa sana ndugu zangu Waislam watakaokwenda kuhiji washindwe kukodi ndege za Air Tanzania kwenda Mecca. 

 

“Mali nyingi za Waislamu ni kweli kabisa zimeporwa, nilianza kulishughulikia hili tangu nikiwa Waziri wa Ardhi. Nilichogundua kwenye mikataba ile, waliohusika kuuza mali za Waislamu ni Waislamu wenyewe. Migogoro yote Duniani huletwa na Shetani, ndugu zangu Watanzania tusimpe nafasi Shetani. Katika Uongozi wangu nashirikiana na Dini zote maana MUNGU wetu ni mmoja.

 

“Waswahili wanasema ‘Mkono mtupu haulambwi na mbwa’, mimi nimekuja na kiasi cha Tsh. milioni 30, nitakukabidhi Mufti wa Tanzania, mkitaka mzigawane ni nyie tu, au mzipangie kazi yoyote,’ amesema Rais Magufuli.

Comments are closed.