Ibada ya Kuaga Miili ya Wafanyakazi 5 wa Azam TV – Video

Magari yenye miili ya marehemu hao yakitoka Muhimbili kuelekea makao makuu ya Azam Media kwa ajili ya kuagwa.

KUFUATIA vifo vya watu saba wakiwemo wafanyakazi watano wa Kampuni ya Azam Media waliofariki dunia jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori, miili ya marehemu hao itaagwa leo katika ofisi za Azam Media, Tabata jijini Dar es salaam.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (mwenye miwani) akiwa pamoja na waombolezaji wengine wakiwemo viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa soka.

“Tulipata taarifa za ajali kutoka kwa wasamaria wema, kwa hali ambayo ilitokea ni kwamba hakukuwa hata na mtu mmoja aliyekuwa katika hali ya kueleza chochote.’ -Tido Mhando – Afisa Mtendaji Azam Media.

Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao akisaini kitabu cha maombolezo.

“Hili ni pigo kubwa sana kwetu sote hasa ukizingatia vijana hawa ambao wametangulia mbele ya haki bado ni wadogo.”-Hamad Masauni – Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.

 

Kwa niaba ya uongozi wa Global Group tunawapa pole AZAM Group, ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu na tunawaombea Mungu awape Nguvu katika kipindi hiki kigumu.

 

“Mioyo ya wanafamilia, watumishi wenzake na Watanzania ambao tumekula matunda ya kazi zao haitaweza kuponywa na neno pole.-Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhaville amefika Makao Makuu ya Azam Media Tabata T.O.T jijini Dar es Salaam, kutoa pole na kisha kuungana na waombolezaji wengine katika kuaga wafanyakazi 5 wa Azam waliofariki kwa ajali ya gari jana Singida.

“Kwenye tasnia ya habari huu ni msiba mwingine mkubwa ndani ya muda mfupi mwaka huu”-Humphrey Polepole – Katibu Mwenezi – CCM.

“Msiba huu umetupiga kwenye tasnia ya habari, kwa sababu mwaka huu umekuwa ni mwaka mgumu sana”-Joyce Mhaville -Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One.

“Ni msiba mzito sana, ni pigo kubwa kwa chombo cha habari na taasisi moja kuondokewa na watu watano kwa mpigo”-January Makamba – Waziri wa Mazingira na Muungano.

“Msiba huu sio wa Azam ni msiba wa kitaifa umemgusa kila mtu”-Mussa Hassan Zungu.

“Nchi nzima imeingia kwenye majonzi kufuatia ajali iliyotokea, mimi kama Mbowe na chama chetu tunaungana na familia za marehemu kuwaombea”-Mhe.Freeman Mbowe.

“Ni jambo ambalo linauma sanaa, lakini ndio maamuzi ya Mwenyezimungu kwa hiyo inakuwa ni shida, sisi inatubidi tuweze kuyakubali”-Prof Ibrahim Lipumba

Mtoto Ethan Florence Ndibalema akiwa na mama yake. Ethan ni mtoto wa marehemu Florence Ndibalema.

“Tunapoteza vijana, Inasikitisha, Inatisha na Inaumiza sana”-Joyce Mhaville -Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One.

“Tumeshtushwa nawapa pole Azam kwa msiba huu mkubwa”-Dkt.Ayoub Rioba -Mkurugenzi wa TBC.

Regina Mengi akisaini kitabu cha maombolezo.

TAZAMA LIVE TUKIO ZIMA


Loading...

Toa comment