The House of Favourite Newspapers

Kamanda Mkondya: Uchaguzi 2020, Hatutapendelea chama chochote – Video

0

 

Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi nchini, DCP Lukas Mkondya (kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi za Makampuni ya Global Group. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa Mtendaji wa Global publisher’s, Saleh Ally.

 

JESHI la Polisi nchini limesema limejipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, utafanyika kwa haki na amani.

Pia limeahidi kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi chote cha uchaguzi huo bila kupendelea chama chochote cha siasa nchini.

DCP Mkondya (kulia) akisamiliana na Mkuregenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (kushoto), Anayefuata kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, SACP Lazaro Mambosasa. Viongozi hao wa polisi wametembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Januari 8, 2020 na Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi nchini, DCP Lukas Mkondya katika mahojiano maalumu na Radio namba moja ya mtandaoni nchini, +255 Global Radio, alipotembelea ofisi za Makampuni ya Global Group zilizopo Sinza Mori, Dar.

DCP Mkondya ambaye aliambatana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, SACP Lazaro Mambosasa, alimwakilisha IGP Simon Sirro.

Shigongo akizungumza na Kamanda Mkondya pamoja na Mambosasa ofisini kwake.

 

Katika ziara hiyo, Makamanda hao walitembelea vitengo mbalimbali vya makampuni ya Global Group kuanzia idara  ya uzalishaji wa Magazeti Pendwa; Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi Mchanganyiko, Risasi na Jumamosi, Global TV Online na Global Digital.

Mhariri Kiongozi wa Global Publishers, Richard Manyota (kushoto) akifafanua namna idara ya magazeti pendwa inavyofanya kazi. Katikati ni DCP Mkondya na SACP Mambosasa (kulia).

 

 

“Jeshi la Polisi hatupendelei CCM wala chama chochote kingine cha siasa, kazi yetu ni kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, tunahakikisha sheria za nchi zinatekelezwa na kusimamiwa bila upendeleo. Ukifanya uhalifu tutakushughulikia bila kujali chama chako cha siasa.

 

Makamanda hao wakiwa na viongozi wa Global Group, Meneja Mkuu Abdallah Mrisho (kushoto) na Mhariri Mtendaji, Saleh Ally.

“Tunafahamu mwaka huu tunakabiliwa na uchaguzi mkuu, tumejipanga vizuri, wananchi msiwe na hofu, kila mtu  akatekeleze haki yake ya kidemokrasia ya kuchagua kiongozi anayemtaka, kila mtu azingatie hali ya amani na utulivu. Uhuru bila sheria ni uendawazimu, tufuate sheria kwa utaratibu, ukifanya kazi nje ya hapo lazima tutakushughulikia.

 

DCP Mkondya akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Championi Ijumaa, John Joseph.

“Tunapenda kutoa shukrani sana kwa wananchi wamekuwa wakishirikiana sana na jeshi la polisi kufichua mambo mbalimbali ya uhalifu. Polisi pekee hawawezi kufika kila sehemu, lakini wananchi wanafahamu maovu mengi yanayofanyika huko na wamekuwa wakitupatia taarifa na sisi tunazifanyia kazi na kuwakamata wahusika kisha kuwafikisha kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.

Makamanda hao wakifafanuliwa jambo na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia na Mawasiliano (IT), Edwin Lindege.

 

“Changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni makosa ya ubakaji, mauaji, kujichukulia sheria mkononi. Sisi kama Jeshi la Polisi tumejipanga kutoa elimu kwa wananchi.. haya mambo wayakatae, wamrudie Mungu kwa dini zao ili waachane na haya mambo maovu kwa sababu ni kinyume cha sheria,” amesema Kamanda Mkondya.

 

Mhariri wa Video wa Global TV Online, Robert Julius akiwaelekeza jambo Makamanda hao.

 

 

Mkuu wa Kitengo cha Global TV Online, Kelvin Nyorobi (kulia) akiwapa maelezo ya namna ambavyo Global TV inafanya kazi zake kushirikiana na vitengo vingine ndani ya ofisi hizo.

 

DCP Mkondya akiwa katika Studio za +255 Global Radio.

 

DCP Mkondya na ASCP Mambosasa wakiwa na watangazaji wa Globla Radio na Global TV Online, Lukas Masungwa na Kisa Daniel baada ya mahojiano ndani ya studio za +255 Global Radio.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL  

Kamanda MKONDYA, MAMBOSASA Waanika HADHARANI Mipango Ya Jeshi La POLISI 2020 l Global Radio

Leave A Reply