Kamati Kuu CCM Yatoa Siku 7 Sakata la Membe, Kinana na Makamba

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyoketi Chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt John Magufuli imepokea taarifa ya awali ya kamati ya Usalama na Maadili juu ya utekelezaji wa wito wa kuhojiwa kwa Abdulrahman Kinana, Yusuf Makamba na Bernad Membe.

Kamati hiyo imetoa siku saba kwa Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu kukamilisha taarifa ya kuwahoji makada wake Yusuph Makamba, Abdulrahman Kinana na Benard Membe na kuiwasilisha kwa Kamati hiyo kwa ajili ya Maazimio.

Makada hao wote wameshafika na kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu.

 

 
Toa comment