The House of Favourite Newspapers

SIMANZI YATAWALA KUAGWA KWA MIILI YA WANAJESHI 3 LUGALO – VIDEO

MAMIA ya waombolezaji wamejoteka kuaga miili ya askari watatu  waliofariki kwa tarehe tofauti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika ya Kati (CAR) wakiwa kwenye jukumu la Ulinzi wa Amani baada ya kushambuliwa na vikundi vinavyosadikiwa kuwa ni vya waasi.

 

Tukio la kuaga wapiganaji hao limefanyika leo Ijumaa, Novemba 23, 2018 katika Viwanja vya Hospitali ya Jeshi, Lugalo vilivyopo Mwenge, Jijini Dar es salaam kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.

Viongozi mbalimbali wa Jeshi na serikali wamehudhuria katika kuaga miili ya askari hao waliyokuwa wakishiriki Ulinzi wa Amani ndani na nje ya Bara la Afrika.

 

Maaskari waliouwawa ni Koplo Mohamed Mussa, Koplo Erick Masauri John na Praiveti Musa Shija Machibya. Mungu azilaze Roho za Mashujaa wetu mahali pema Peponi, Amina.

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.