The House of Favourite Newspapers

JPM Aamuru Mgambo JKT Kurudisha Eneo la Ekari 50

0
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameamuru eneo la ekari 50 lililopo Mkata mkoani Tanga ambalo walipewa Mgambo JKT miaka saba iliyopita kwa ajili ya kujenga kiwanda na wakashindwa kuliendeleza, walirudishe haraka kwa serikali ya kijiji ili lipangiwe matumizi mengine.

 

Hayo ameyasema leo wakati akiwa njiani kuelekea Tanga kwa ajili ya kumpokea mgeni wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ambapo kesho wataweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Kaskazini mwa Tanga.

 

Rais Magufuli amekuwa akisisitiza kuwa wawekezaji au taasisi itakayopewa eneo kwa ajili ya kujenga kiwanda lazima ifanye hivyo, kushikilia eneo bila kuliendeleza kutasababisha mhusika anyang’anywe eneo hilo na apewe mwingine mwenye uwezo wa kuliendeleza.

 

Aidha rais ametoa onyo kwa viongozi waliohusika kuhujumu kwa kujinufaisha na fedha kiasi cha Tsh milioni 500 za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Handeni Vijijini kuwa wajiandae kuzirudisha ama kwenda gerezani.

Pia Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ummy Mwalimu kuunda tume ya kuchunguza ubadhilifu wa fedha hizo.

 

MTAZAME RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA HAPA

Leave A Reply