The House of Favourite Newspapers

LIVE KUTOKA KAITABA: KAGERA SUGAR 1-2 YANGA (FULL TIME)

0
MPIRA UMEKWISHAAAAA
SUB Dk 90+3 Yanga wanamtoa Chirwa na nafasi yake inachukuliwa na kinda Edward Maka Dk 90+1 shuti la Ludovick lakini Rostande anakuwa makini na kudaka

DAKIKA ZA NYONGEZA
Dk 89 krosi nzuri, kipa Rostande anabaki langoni na Kagera wenyewe wanapoteza nafasi
Dk 87, Ajibu anapiga mkwaju wa adhabu hapa lakini ni dhaifu

Dk 85 Ajibu anachonga kona chinichini,  lakini Yanga wanafanyiwa madhambi
Dk 85 Inachongwa safi na Juma Abdul, Kagera wanaokoa na kuwa kona tena
Dk 84 Yanga wanafanya shambulizi la kushitukiza, anamtoka Nyosso lakini Nyosso tena anafanikiwa kuokoa na kuwa kona
Dk 83 Yanga wanaonekana kuimarisha ulinzi zaidi ikiwezekana watoke na ushindi huo wa mbili moja
KADI Dk 78 Chirwa analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe
Dk 78 bado mpira unachezwa katikati ya uwanja zaidi na Yanga kiasi fulani wanaonekana kurejea nyuma wengi zaidi ingawa linaweza kuwa jambo baya kwao
Dk 73 mpira wa adhabu wa Kibaya, hatari kabisa, Rostande anapangua kwa ujuzi wa juu na kuwa kona, Yanga wanaokoa

KADI Dk 72 Mwamuzi Shamba anamlamba Yonzani kadi ya njano kwa kucheza kindava
Dk 70 Kaseja anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira safi wa krosi ya Ajibu aliyemtoka beki pembeni
Dk 68, Kagera Sugar wanaonekana kufika zaidi kwenye lango la Yanga lakini hawana mipango
SUB Dk 64 Themi Felix anaingia kuchukua nafasi ya Edward Christopher
SUB Dk 62 Yanga inamtoa Mwashiuya na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 61 mpira unaonekana uko ndani ya nyavu za Kagera, lakini mwamuzi Andrew Shamba anaonekana uko makini kwa kuwa nyavu zimechanika, goal kick
SUB Dk 57 Yanga wanafanya mabadiliko kwa kumtoa Makapu na nafasi yake inachukuliwa na Raphael Daud

Dk 55 Kibaya yuko chini akitibiwa baada ya kuumia
GOOOOOOOO Dk 52 Kibaya hatimaye anafanikiwa kufunga bao la kichwa kwa kosa la kipa Rostande ambaye alichelewa lakini hakuinua mikono
Dk 50, kona ya Mwashiuya lakini Nyosso anaokoa kibabe hapa
GOOOOOOOOOO Dk 48, Ajibu anaifungia Yanga bao safi la pili akipachika mpira pembeni kulia mwa Kaseja
Dk 47, Nyosso anamuweka chini Chirwa hapa wakati wakiwania mpira
Dk 45, kipindi cha pili kimeanza na Kagera wanaonekana wamepanga kusawazisha bao ili kudanya hesabu za haraka

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
KADI Dk 45, Edward Christopher analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ajibu aliyekuwa anamnyanyasa
Dk 44 wanachofanya sasa Yanga ni kuyapoza mashambulizi kwenda upande wao
Dk 42, shuti kali la mpira wa adhabu la Jaffar Kibaya linatoka sentimeta chache nje ya lango la Yanga
GOOOOOOOOOO Dk 39 pasi nzuri ya Ajibu, Chirwa anageuka vizuri na kufunga bao safi la kwanza kwa Yanga leo la kwanza kwake msimu huu
Dk 38, Ajibu pembeni ya uwanja anajaribu vizuri lakini goal kickDk 37, krosi safi ya Juma Abdul, Kagera Sugar wanaokoa na kuwa kona, inachongwa wanaokoa

Dk 36, Tshishimbi anageuka vizuri lakini shuti lake linakuwa nyanya kwa Kaseja
Dk 34, Yanga wanaonekana kubadilika, Chirwa anaingia vizuri kabisa lakini NYosso anaokoa
Dk 29, Buswita anajaribu shuti la mbali lakini linakuwa nyanya kwa Kaseja
Dk 26 Kaseja bado anatibiwa pale ndani ya uwanja
Dk 24, krosi ya Mwashiuya, Nyosso anafanya kazi ya ziada kuokoa na inakuwa kona. Inachongwa, Kagera wanaokoa lakini Kaseja yuko chini
Dk 20, Kibaya anampiga kanzu beki wa Yanga na kuachia mkwaju mkali kabisa, unatoka sentimeta chache na lango la Yanga
Dk 17 mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja kwa kila upande

Dk 15, Yondani anaonyesha ukongwe wake katika ulinzi, anamdhibiti Kibaya na mwamuzi anasema Yondani amechezewa madhambi
Dk 11, Tshishimbi tena anafanya kazi nzuri kwa kutoa pasi nne mfululizo akigongeana na wenzake, lakini Nyosso anakuwa makini, anaokoa
Dk 9, Jaffar Kibaya katika nafasi nzuri lakini mpira wake wa kichwa haukulenga lango
Dk 7, Tshishimbi ambaye anacheza namba nane anaonekana kuchachafya katikati ya uwanja
Dk 4 krosi safi ndani ya lango la Yanga, lakini kipa Youthe anakuwa mwepesi na kuuwahi mpira

Dk 1, mechi imeanza kwa kasi na inaonekana Kagera Sugar wanataka kupata bao la haraka.
Leave A Reply