The House of Favourite Newspapers

Lulu Kortini Tena Leo Kesi ya Kifo cha Kanumba – Video

0

MSANII wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo Ijumaa, Oktoba 20, amefika katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili ya kusababisha kifo cha aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia.

Jana mahakamani hapo, Mdogo wa Kanumba, Seth alitoa ushahidi wake akiieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro kati ya Lulu na Kanumba aliousikia ambapo Lulu alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo na Kanumba.

Leo mashahidi watatu wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kwenye kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.

VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply